Recent comments

Breaking News

BANNER 728X90

Zari arudi Afrika Kusini baada ya kuruhusiwa kuishi kwa nyumba ya Ivan Ssemwanga

Zari arudi Afrika Kusini baada ya kuruhusiwa kuishi kwa nyumba ya Ivan Ssemwanga

Kamati ya kuangalia jinsi mali aliyoacha Ivan inatumika ilibuniwa baada ya familia ya mwenda zake kugundua kuwa hakuwacha Will yoyote ambayo ingeeleza jinsi ambavyo mali yake ingegawanywa.
Wanachama wa kamati hio ni; Zari, Ritah Ssemwanga (dadake Ivan), George Ssemwanga Pinto (kakake Ivan), na Lawrence Kiyingi Muyanja maarufu kama King Lawrence (rafike yake Ivan).
Kamati hio iliamua kuwa Zari asimamie shule za Ivan huku Afrika Kusini. Katika kikao kilichoandaliwa Jumamosi, kamati hio pia iliamua kumpa Zari nyumba moja Afrika Kusini ambayo ataishi na wanawe watatu aliyowazaa na Ivan.
Zari aliondoka Uganda kuelekea Afrika Kusini baada ya kamati hio kuamua jinsi mali ya Ivan itakavyogawanywa. Kamati hio itabaki kuwa na mamlaka ya kuamua jinsi mali ya Ivan itatumika mbaka wanawe watatu watakapotimia umri ya miaka 18.
Sasa haijulikani kama Zari atabaki kuishi kwa nyumba ya Ivan Pretoria ama ataenda kuishi na wanawe watatu kwa nyumbo aliyonunua Diamond Platnumz kule Johannesburg.

No comments