Recent comments

Breaking News

BANNER 728X90

Msanii wa Bongo AT asimulia ugomvi wa Diamond Platnumz na Alikiba ulipoanzia

Msanii wa Bongo AT asimulia ugomvi wa Diamond Platnumz na Alikiba ulipoanzia

Ni wengi bado wanajiuliza ni nini kilichotokea Kati ya Diamond Platnumz na Alikiba kuwafanya wawili hao kukosana.
AT ambaye ni maarufu Bongo alisimulia tukio la Kiba na Naseebu akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muimbaji huyo maarufu wa muziki wa mduara alisema;
“Tulikuwepo tupo Oman kwenye hotel moja inaitwa Dream tulikuwa tuna show, kwa hiyo walikuwa wanacheza game, Alikiba amechagua Real Madrid na Diamond Barcelona, mimi nimekaa pembeni naangali watu wanacheza game yao. Ali akawa amefungwa mbili, akawa anataka kupiga free kiki kwenye game Diamond akamsukuma akamwambia halafu mwanangu nakutafuta siku nyingi. Alikiba akanyanyuka ikabidi na mimi ninyanyuke sasa, nikamuuliza Ali tatizo nini mbona kama mnataka kupigana halafu tupo ugenini wazee vipi?  Akaniambia huyo dogo kuna vitu anavifanya mimi sijavipenda.”
Aliendelea kwa kusema,
“Mwisho wa siku naona kama vile vitu vinaendelea halafu watu wanakurupuka wala tatizo wao hawalijui. Ebu watafute ukweli ulipo, sijui huyo kamtoa kwenye wimbo huyo, kuna jambo lingine ambalo lipo. Kiukweli kuna vitu ambavyo pengine wao wenyewe wanavijua ni vikubwa zaidi,”

No comments