UN: Rwanda inachochea machafuko Kongo DRC

Maafisa wa kijeshi wa Rwanda wanachochea machafuko huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hayo yameelezwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa. Ripoti ya siri ya kurasa 43 ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa kundi la waasi la Machi 23 linaendelea kuwaandikisha wapiganaji kutoka nchi jirani ya Rwanda kwa msaada wa maafisa wa kijeshi wa nchi hiyo. Juni 14 mwaka huu kundi hilo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa liliitumia barua serikali ya Kigali likiitaka itoe maelezo kuhusu uungaji mkono wake katika uwanja huo.
Kundi hilo limewasilisha ripoti hiyo kwa kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa mara kadhaa umezituhumu nchi za Rwanda na Uganda kwa kuwaunga mkono waasi huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment